Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa kipimo cha mwaka unapima kiwango cha kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma zote zinazotumiwa na kaya binafsi.

Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa mwaka ulioishia mwezi Januari, 2022 umepungua hadi asilimia 4.0 kutoka asilimia 4.2 kwa mwaka ulioishia mwezi Desemba, 2021.

Hii inamaanisha kuwa, kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia mwezi Januari, 2022 imepungua ikilinganishwa na kasi iliyokuwepo kwa mwaka ulioishia mwezi Desemba, 2021. Fahirisi za Bei zimeongezeka kutoka 101.53 mwezi Januari, 2021 hadi 105.59 mwezi Januari, 2022.

Bonyeza hapa kupata Mfumuko wa Bei kwa mwezi January,2022