Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa kipimo cha mwaka unapima kiwango cha kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma zote zinazotumiwa na kaya binafsi. Jedwali Namba 1 linaonesha kuwa, Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa mwaka ulioishia mwezi Februari, 2022 umepungua hadi asilimia 3.7 kutoka asilimia 4.0 kwa mwaka ulioishia mwezi Januari, 2022. Hii inamaanisha kuwa, kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia mwezi Februari, 2022 imepungua ikilinganishwa na kasi iliyokuwepo kwa mwaka ulioishia mwezi Januari, 2022. Fahirisi za Bei zimeongezeka kutoka 102.44 mwezi Februari, 2021 hadi 106.20 mwezi Februari, 2022.

Bonyeza hapa kupata Mfumuko wa Bei kwa mwezi Februari,2022