Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa kipimo cha mwaka unapima kiwango cha kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma zote zinazotumiwa na kaya binafsi.

Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa mwaka ulioishia mwezi Aprili, 2022 umeongezeka hadi asilimia 3.8 kutoka asilimia 3.6 kwa mwaka ulioishia mwezi Machi, 2022.

Hii inamaanisha kuwa, kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia mwezi Aprili, 2022 imeongezeka ikilinganishwa na kasi iliyokuwepo kwa mwaka ulioishia mwezi Machi, 2022. Fahirisi za Bei zimeongezeka kutoka 103.95 mwezi Aprili, 2021 hadi 107.88 mwezi Aprili, 2022.

 Bonyeza hapa kupata Mfumuko wa Bei kwa mwezi Aprili,2022