Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa mwaka ulioishia mwezi Septemba, 2022 umeongezeka hadi asilimia 4.8 kutoka asilimia 4.6 kwa mwaka ulioishia mwezi Agosti, 2022. Hii inamaanisha kuwa, kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia mwezi Septemba, 2022 imeongezeka ikilinganishwa na kasi iliyokuwepo kwa mwaka ulioishia mwezi Agosti, 2022. Fahirisi za Bei zimeongezeka kutoka 103.71 mwezi Septemba, 2021 hadi 108.73 mwezi Septemba, 2022.

Bonyeza hapa kupata Mfumuko wa Bei kwa mwezi Septemba,2022.