Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa kipimo cha mwaka unapima kiwango cha kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma zote zinazotumiwa na kaya binafsi.

Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa mwaka ulioishia mwezi Oktoba, 2022 umeongezeka hadi asilimia 4.9 kutoka asilimia 4.8 kwa mwaka ulioishia mwezi Septemba, 2022. Hii inamaanisha kuwa, kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia mwezi Oktoba, 2022 imeongezeka ikilinganishwa na kasi iliyokuwepo kwa mwaka ulioishia mwezi Septemba, 2022. Fahirisi za Bei zimeongezeka kutoka 103.61 mwezi Oktoba, 2021 hadi 108.73 mwezi Oktoba, 2022.

Bonyeza hapa kupata Mfumuko wa Bei kwa mwezi Oktoba,2022.