Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa kipimo cha mwaka unapima kiwango cha kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma zote zinazotumiwa na kaya binafsi.

Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa mwaka ulioishia mwezi Novemba, 2022 umebaki katika asilimia 4.9 kama ilivyokuwa kwa mwaka ulioishia mwezi Oktoba, 2022.

Hii inamaanisha kuwa, kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia mwezi Novemba, 2022 imekuwa sawa na kasi iliyokuwepo kwa mwaka ulioishia mwezi Oktoba, 2022. Fahirisi za Bei zimeongezeka kutoka 104.08 mwezi Novemba, 2021 hadi 109.16 mwezi Novemba, 2022.

Bonyeza hapa kupata Mfumuko wa Bei kwa mwezi Novemba,2022.