Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa kipimo cha mwaka unapima kiwango cha kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma zote zinazotumiwa na kaya binafsi.

Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa mwaka ulioishia mwezi Februari, 2023 umepungua kidogo hadi asilimia 4.8 kutoka asilimia 4.9 kwa mwaka ulioishia mwezi Januari, 2023.

Hii inamaanisha kuwa, kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia mwezi Februari, 2023 imepungua ikilinganishwa na kasi iliyokuwepo kwa mwaka ulioishia mwezi Januari, 2023. Fahirisi za Bei zimeongezeka kutoka 106.20 mwezi Februari, 2022 hadi 111.28 mwezi Februari, 2023.

Bonyeza hapa kupata Mfumuko wa Bei kwa mwezi Februari,2023.