Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa kipimo cha mwaka unapima kiwango cha kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma zote zinazotumiwa na kaya binafsi. Jedwali Namba 1 linaonesha kuwa, Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa mwaka ulioishia mwezi Machi, 2023 umefika asilimia 4.7 kutoka asilimia 4.8 kwa mwaka ulioishia mwezi Februari, 2023. Hii inamaanisha kuwa, kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia mwezi Machi, 2023 imepungua kidogo ikilinganishwa na kasi iliyokuwepo kwa mwaka ulioishia mwezi Februari, 2023. Fahirisi za Bei zimeongezeka kutoka 107.09 mwezi Machi, 2022 hadi 112.13 mwezi Machi, 2023.

Bonyeza hapa kupata Mfumuko wa Bei kwa mwezi Machi,2023.