Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa kipimo cha mwaka unapima kiwango cha kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma zote zinazotumiwa na kaya binafsi.

Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa mwaka ulioishia mwezi Septemba, 2023 umebaki katika asilimia 3.3 kama ilivyokuwa kwa mwaka ulioishia mwezi Agosti, 2023.

Hii inamaanisha kuwa, kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia mwezi Septemba, 2023 imebaki kuwa sawa na kasi iliyokuwepo kwa mwaka ulioishia mwezi Agosti, 2023. Fahirisi za Bei zimeongezeka kutoka 108.73 mwezi Septemba, 2022 hadi 112.35 mwezi Septemba, 2023.

Bonyeza hapa kupata Mfumuko wa Bei kwa mwezi Septemba,2023