Pato la Taifa ni thamani ya bidhaa na huduma zinazozalishwa Nchini katika kipindi husika. Pato la Taifa hutumika kutathmini ukuaji wa uchumi katika mwaka husika. Taarifa hii ni kwa kipindi cha kuanzia mwezi Januari hadi Desemba, 2017.

Taarifa zilizotumika kutayarisha takwimu za Pato la Taifa  kwa mwaka 2017 zimetokana na uzalishaji wa bidhaa na huduma Nchini katika kipindi cha Januari hadi Desemba 2017 kutoka vyanzo mbalimbali vya takwimu rasmi kutoka katika Wizara, Idara na Taasisi za Serikali. Aidha, ukokotoaji wa takwimu za Pato la Taifa umezingatia matakwa ya Mfumo wa Umoja wa Mataifa wa mwaka 2008 (United Nations, System of National Accounts 2008).

Thamani ya Pato la Taifa kwa bei za soko za miaka husika katika mwaka 2017 iliongezeka na kufikia shilingi trilioni 116.1 kutoka shilingi trilioni 103.1 mwaka 2016. Aidha, thamani ya Pato la Taifa kwa bei ya soko ya mwaka 2007 zilikuwa shilingi trilioni 50.5 mwaka 2017 kutoka shilingi trilioni 47.1 mwaka 2016, ambayo ni sawa na ongezeko la asilimia 7.1.

Bonyeza hapa kupata Taarifa Kamili ... (PDF)