Pato la Taifa kwa bei za mwaka 2015 katika kipindi cha Julai hadi Septemba 2019 liliongezeka kwa kasi ya asilimia 6.8 ambapo thamani ya bidhaa na huduma iliongezeka hadi shilingi trilioni 28.6 mwaka 2019 kutoka shilingi trilioni 26.8 katika kipindi kama hicho mwaka 2018.

Aidha, Pato la Taifa kwa bei za miaka husika lilikuwa na thamani ya shilingi trilioni 32.2 katika kipindi husika ikilinganishwa na shilingi trilioni 30.5 katika kipindi kama hicho mwaka 2018.

Taarifa zilizotumika kutayarisha takwimu za Pato la Taifa Robo ya tatu (Julai- Septemba) ya Mwaka 2019 zilikusanywa kutoka katika shughuli zote za uchumi za uzalishaji wa bidhaa na huduma zilizofanyika nchini katika kipindi hicho.  Pia, ukokotoaji umezingatia matakwa ya Mfumo wa Umoja wa Mataifa wa Takwimu za Pato la Taifa unaojulikana kama System of National Accounts 2008.

Bonyeza HAPA kusoma Muhtasari wa Taarifa ya Pato la Taifa Robo ya Tatu 2019 (pdf)