Muhtasari huu unatoa taarifa za awali za Pato la Taifa kwa bei za miaka husika na bei za mwaka wa kizio wa 2015 kwa Tanzania Bara. Taarifa za Pato la Taifa kwa robo mwaka hutumika kutathmini mabadiliko ya kiuchumi katika vipindi vifupi na kuwezesha kutayarisha sera za kiuchumi kwa wakati muafaka

Katika kipindi cha robo ya nne (Oktoba - Desemba) ya mwaka 2020, thamani ya Pato la Taifa kwa bei za miaka husika ilikuwa shilingi trilioni 41.4 ikilinganishwa na shilingi trilioni 38.9 katika kipindi kama hicho mwaka 2019. Vile vile, thamani ya Pato la Taifa kwa bei za mwaka 2015 iliongezeka hadi shilingi trilioni 35.2 katika robo ya nne ya mwaka 2020 kutoka shilingi trilioni 33.5 katika kipindi kama hicho mwaka 2019 sawa na ukuaji wa asilimia 4.9.

Kusoma zaidi bonyeza hapa