Pato la Taifa katika kipindi cha Robo ya Kwanza ya mwaka 2022 (Januari - Machi), kwa bei za miaka husika liliongezeka hadi shilingi trilioni 43.4 kutoka shilingi trilioni 38.9 kipindi kama hicho mwaka 2021. Aidha, katika kipindi hicho, Pato Halisi la Taifa liliongezeka hadi shilingi trilioni 34.9 kutoka shilingi trilioni 33.1 katika kipindi kama hicho mwaka 2021 sawa na ukuaji wa asilimia 5.4.

Bonyeza hapa kupakua ripoti nzima