Utafiti wa Viashiria na Matokeo ya UKIMWI nchini Tanzania ni utafiti wa kitaifa uliofanyika katika ngazi ya kaya kuanzia mwezi Oktoba, 2016 mpaka mwezi Agosti, 2017 ili kujua hali ya maambukizi ya Virusi Vya UKIMWI (VVU) kitaifa. Utafiti huu ulitoa huduma za ushauri nasaha, upimaji wa VVU na utoaji wa majibu pia ulikusanya taarifa za kaya na taarifa binafsi za wanakaya, upatikanaji wa huduma na matibabu kwa watu wanaoishi na VVU. Utafiti huu uliopima maambukizi mapya ya VVU na kiasi cha VVU mwilini kwa watu wanaoishi na VVU ni wa kwanza kufanyika nchini. Matokeo ya utafiti huu yanatoa taarifa katika ngazi ya kitaifa na mikoa kwa ajili ya ufuatiliaji wa udhibiti wa VVU.

Bonyeza Hapa kupata Matokeo kwa Ufupi ya Utafiti wa Viashiria na Matokeo ya UKIMWI wa 2015/16