Matokeo ya Sensa ya kilimo ya mwaka 2019/20 yanaonesha kuwa kati ya kaya 12,007,839 zilizopo Tanzania (11,659,589 Tanzania Bara na 348,250 Tanzania Zanzibar), kaya 7,837,405 (asilimia 65.3) zinajihusisha na shuguli za kilimo. Kati ya hizo, kaya 5,088,135 (asilimia 64.9) zimejihusisha na kilimo cha mazao tu, ikifuatiwa na kaya 2,589,156 (asilimia 33.0) ambazo zilijikita katika kilimo cha mazao pamoja na ufugaji na idadi ndogo ya kaya (chini ya asilimia moja) zilijihusisha na ufugaji wa samaki na ufugaji wa kuhamahama

Kaya 7,657,185 sawa na asilimia 65.7 ya kaya zilizopo Tanzania Bara zinajihusisha na shughuli za kilimo, kati ya hizo, kaya 4,972,373 sawa na asilimia 64.9 zinajihusisha na kilimo cha mazao pekee, ikifuatiwa na kaya 2,526,846 (asilimia 33.0) zinazojihusisha na kilimo cha mazao na ufugaji, asilimia 2 wanajishughulisha na mifugo tu na idadi ndogo ambayo ni chini ya asilimia moja zinajihusisha na ufugaji wa samaki pamoja na ufugaji wa kuhamahama.

Kwa upande wa Tanzania Zanzibar, kaya 180,220 (asilimia 51.8) zinajihusisha na shughuli za kilimo, kati ya hizo, kaya 115,762 (asilimia 64.2) zimejihusisha na kilimo cha mazao pekee ikifuatiwa na kaya 62,310 (asilimia 34.6) zinazojihusisha na kilimo cha mazao na ufugaji. Aidha, kaya 2,149 (asilimia 1.2) zilijihusisha na shughuli za mifugo tu

Bonyeza hapa kusoma taarifa kamili

Bonyeza hapa kupakua nakala yako