Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) kwa kushirikiana na Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekekezaji (MITI) ilifanya Utafiti wa mwaka wa Uzalishaji Viwandani kwa miaka rejea ya 2015 na 2016.

Mwaka 2015 jumla ya viwanda vilivyofanya uzalishaji vilikuwa 2,389. Kati ya viwanda 2,389 , sekta ndogo ya utengenezaji wa bidhaa viwandani ilikuwa na viwanda vingi (1,864, asilimia 78.0) kuliko sekta ndogo yoyote, ikifuatiwa na sekta ndogo ya uchimbaji madini na mawe viwanda (384, asilimia 16.1), kukusanya, kutibu na kusambaza maji viwanda (110, asilimia 4.6) na ya mwisho ilikuwa uzalishaji na usambazaji wa umeme, gesi, mvuke na kubadilisha hali (joto/baridi) ambayo ilikuwa na viwanda(31, asilimia 1.3).

Kwa mwaka 2016 jumla ya viwanda vilivyofanya uzalishaji vilikuwa 2,462. Kati ya viwanda 2,462 , sekta ndogo ya utengenezaji wa bidhaa viwandani ilikuwa na viwanda vingi (1,931, asilimia 78.4) kuliko sekta ndogo yoyote, ikifuatiwa na sekta ndogo ya uchimbaji madini na mawe viwanda (385, asilimia 15.6), kukusanya, kutibu na kusambaza maji viwanda (110, asilimia 4.5) na ya mwisho ilikuwa uzalishaji na usambazaji wa umeme, gesi, mvuke na kubadilisha hali (joto/baridi) ambayo ilikuwa na viwanda(36, asilimia 1.5).

Bonyeza Hapa Kwa Taarifa nzima ya Utafiti wa mwaka wa Uzalishaji Viwandani 2015 na 2016