Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania itafanya Sensa ya Watu na Makazi Mwezi Agosti Mwaka 2022. 

Maandalizi ya Sensa hiyo yanafanyika kwa mujibu wa Sheria ya Takwimu SURA 351.

Uzinduzi huu utafanyika katika Viwanja vya Ofisi ya Taifa ya Takwimu vilivyopo Barabara ya Jakaya Kikwete karibu na Ukumbi wa Mikutano wa Chama Cha Mapinduzi wa Jakaya Kikwete Convention Centre jijini Dodoma.

Matangazo ya uzinduzi huo yatarushwa moja kwa moja kupitia Televisheni ya Taifa- TBC pamoja na mitandao mbalimbali ya Kijamii kuanzia saa mbili na nusu asubuhi.