Kitabu cha Takwimu za Msingi cha Tanzania mwaka 2020 kinatoa picha ya hali ya uchumi, jamii, mazingira na siasa kwa ujumla. Kitabu hiki kina takwimu kuanzia mwaka 2016 mpaka mwaka 2020. Kitabu hiki kina takwimu ambazo ni za kiujumla kutoka vyanzo mbali mbali vya takwimu rasmi yakiwemo machapisho yanatolewa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Wizara, Taasisi na Wakala wa Serikali. Takwimu zilizowasilishwa ni muhimu kwa watunga sera kwa ajili ya kupanga, kufuatilia na kuratibu mipango anuwai ya maendeleo katika ngazi zote.

Bonyeza kusoma Kitabu cha Takwimu za Msingi cha Tanzania mwaka 2020

Bonyeza hapa kupakua Kitabu cha takwimu za Msingi cha Tanzania mwaka 2020