Utafiti wa Viashiria vya Malaria Tanzania wa mwaka 2017 (2017 MIS) 

2017MIS a7f1b

Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) kwa kushirikiana na Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto – Tanzania Bara na Wizara ya Afya – Zanzibar inafanya Utafiti wa Viashiria vya Malaria Tanzania wa mwaka 2017 (2017 MIS). Utafiti huu unahusisha kaya binafsi na unatumia sampuli wakilishi ya Kitaifa, Kimkoa na ngazi ya Kitaifa kwa maeneo ya Mijini na Vijijini.

Taarifa zinazokusanywa katika utafiti huu zitasaidia katika kufuatilia na kutathmini mipango mbalimbali ya Kitaifa ili kuweza kutoa huduma bora za afya hususan zinazohusiana na malaria.

Chagua HAPA kupakua madodoso ya Utafiti huu.