Utafiti Wa Kutathmini Utoaji Wa Huduma Za Afya Nchini Wa Mwaka 2014/2015

Utafiti wa Kutathmini Utoaji wa Huduma za Afya Nchini Tanzania (TSPA) wa mwaka 2014-15 ni wa pili kufanyika nchini. Utafiti wa kwanza ulifanyika mwaka 2006. Utafiti huu umefanyika Tanzania Bara na Tanzania visiwani.

Utafiti ulikusudia kukusanya taarifa kutoka katika sampuli ya vituo vyote vinavyotoa huduma ya afya nchini na kuangalia utayari wa vituo hivyo kutoa huduma bora ya afya ya mtoto, uzazi wa mpango, afya ya uzazi na mtoto mchanga, VVU, magonjwa yatokanayo na ngono, magonjwa yasiyoambukiza na kifua kikuu.

Yafuatayo ni matokeo ya utafiti wa kutathmini utoaji wa huduma za afya nchini wa mwaka 2014/2015. 

  1. Matokeo muhimu ya Utafiti wa kutathmini utoaji wa huduma za Afya nchini wa mwaka 2014/2015.
  2. Chati za ukutani ikionesha matokeo ya Utafiti wa kutathmini utoaji wa huduma za Afya nchini wa mwaka 2014/2015
  3. Kipeperushi chenye matokeo ya Utafiti wa kutathmini utoaji wa huduma za Afya nchini wa mwaka 2014/2015
  4. Namna ya kusoma na kuelewa Jedwali la kitakwimu.