OFISI YA TAIFA YA TAKWIMU IMEWASILISHA MATOKEO MUHIMU YA UTAFITI KUHUSU HAKI NA USALAMA WA UMILIKI RASILIMALI ARDHI NA MAKAZI TANZANIA MWAKA 2017/2018

headerdom cc7ea

 

OFISI YA YA TAIFA YATAKWIMU INAPENDA KUWASHUKURU WADAU WOTE MLIOHUDHURIA KWENYE MKUTANO WA UWASILISHWAJI WA MATOKEO YA UTAFITI KUHUSU HAKI NA USALAMA WA UMILIKI WA RASILIMALI ARDHI NA MAKAZI TANZANIA. UTAFITI HUU ULIFANYWA NA OFISI YA GLOBAL LAND ALLIANCE YA MAREKANI NA WASHIRIKA WAKE. OFISI YA TAIFA YA TAKWIMU ILIRATIBU KAZI HIYO NA KUTOA MATOKEO YAKE KAMA MLIVYOSHUHUDIA. UTAFITI HUU ULIFANYIKA TANZANIA BARA NA ZANZIBAR KATI YA MWAKA 2016/17 NA 2017/18 KWA KUFANYA MAHOJIANO NA WATU WENYE UMRI WA MIAKA 18 AU ZAIDI KUPATA MTAZAMO WAO ‘’PERCEPTIONS’’ JUU YA HAKI NA USALAMA WA UMILIKI WA RASILIMALI ARDHI NA MAKAZI.

MATOKEO YALIYOWASILISHWA NI BAADHI TU YA TAARIFA MUHIMU ZILIZOCHAMBULIWA KUTOKA NA DATA ZA MIAKA MIWILI MFULULIZO. BADO OFISI YA TAIFA YA TAKWIMU ITAENDELEA KUSHIRIKIANA NA WADAU WA NDANI NA NJE YA NCHI KUCHAMBUA KWA KINA NA KUSAMBAZA MATOKEO ZAIDI YA UTAFITI HUU KWA MIKOA YOTE NA KIKANDA. MNAKARIBISHWA SANA KUUNGANA NA OFISI YA TAIFA YA TAKWIMU KUFANYA MICHAKATO SHIRIKISHI KUFANIKISHA MATARAJIO HAYA. POKEENI TAARIFA ILIYOWASILISHWA PAMOJA NA HOTUBA YA MHESHIMIWA NAIBU WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI, DKT ANGELINA MABULA (MB) PAMOJA NA HOTUBA YA UTANGULIZI ILIYOTOLEWA NA MKURUGENZI MKUU WA OFISI YA TAIFA YA TAKWIMU DKT. ALBINA CHUWA.

ASANTENI SANA KWA USHIRIKIANO WENU

 

MKURUGENZI MKUU

OFISI YA TAIFA YA TAKWIMU

 

1. BONYEZA HAPA KUSOMA  WASILISHO (PRESENTATION) LA MRADI.

2. HOTUBA YA  MGENI RASMI - NAIBU WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI

3. HOTUBA YA MKURUGENZI MKUU, OFISI YA TAIFA YA TAKWIMU