Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aweka jiwe la msingi katika Jengo la Ofisi ya Takwimu - Dodoma 20 Desemba 2017.

 

jengouzinduzi3 07f9f

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na mwakilishi mkazi wa Benki ya Dunia Bella Bird wakifungua kitambaa cha jiwe la msingi la jengo la ofisi ya Taifa ya Takwimu mkoani Dodoma. Desemba 20, 2017

 

jengouzinduzi5 aa014

Mhe. Dkt. John Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  akizungumza na Waziri Mkuu Mhe. Kassima Majaliwa wakati wa hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi la jengo la ofisi ya Taifa ya Takwimu Dodoma Desemba 20, 2017.

 

jengouzinduzi4 20c60

Rais Dkt. John Pombe Magufuli akipokea ramani yenye takwimu za hali ya maambukizi ya VVU kimkoa kutoka kwa Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango wakati wa hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi jengo la ofisi ya Taifa ya Takwimu mjini Dodoma Desemba 20, 2017.

 

jengouzinduzi7 e0244

Rais Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mwenyekiti wa Bodi ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu Ndugu. Andrew W. Massawe wakati wa hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi la jengo la ofisi ya Taifa ya Takwimu Dodoma Desemba 20, 2017.

 

jengouzinduzi6 d4a46

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Mkurugenzi Mkuu wa NBS, Dkt. Albina Chuwa baada ya kuweka jiwe la msingi katika jengo la ofisi ya Taifa ya Takwimu  Dodoma Desemba 20, 2017.