Pato la Taifa kwa Robo ya Pili ya Mwaka (Aprili-June) 2015

Ofisi ya Taifa ya Takwimu ina jukumu la kukusanya, kuchakata na kusambaza takwimu rasmi nchini ikiwa ni pamoja na takwimu za Pato la Taifa kwa robo Mwaka.

Takwimu za Pato la Taifa kwa robo mwaka ni thamani ya bidhaa na huduma zilizozalishwa nchini katika vipindi vya miezi mitatu mitatu ambavyo ni Januari – Machi, Aprili – Juni, Julai – Septemba na Oktoba - Desemba kwa kutumia taarifa za uzalishaji wa bidhaa na huduma zilizo kusanywa kutoka katika vyanzo mbalimbali nchini ikiwa ni pamoja na taarifa za urari wa mauzo nje ya nchi

Thamani ya Pato la Taifa kwa bei za miaka inayohusika katika kipindi cha Aprili hadi Juni ilikuwa TZS 23.6 trilioni ikilinganishwa na TZS 20.4 trilioni kipindi kama hicho mwaka 2014. Aidha, thamani ya Pato la Taifa kwa bei za mwaka 2007 katika kipindi cha robo mwaka ya pili ilikuwa TZS. 11.1 trilioni kwa mwaka 2015 ikilinganishwa na TZS 10.3 trilioni katika kipindi kama hicho mwaka 2014, hii inamaanisha kuwa Pato la Taifa liliongezeka kwa kasi ya asilimia 7.9 katika kipindi cha robo ya pili mwaka 2015 ikilinganishwa na kasi ya asilimia 10.1 katika kipindi kama hicho mwaka 2014.

Bonyeza hapa kupata Taarifa zaidi ...