CPI Julai 2015 (Kiswahili)

Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa kipimo cha mwaka unapima kiwango cha badiliko la kasi ya bei za bidhaa na huduma zote zinazotumiwa na kaya binafsi.

Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa mwezi Julai, 2015 umeongezeka hadi asilimia 6.4 kutoka asilimia 6.1 ilivyokuwa mwezi Juni, 2015.

Hii inamaanisha kuwa, kasi ya upandaji wa bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia mwezi Julai, 2015 imeongezeka ikilinganishwa na kasi

iliyokuwepo kwa mwaka ulioishia mwezi Juni, 2015. Fahirisi za Bei zimeongezeka hadi 158.78 kwa mwezi Julai, 2015 kutoka 149.16 mwezi Julai, 2014.

Mfumuko wa Bei wa bidhaa za Vyakula na Vinywaji Baridi kwa mwezi Julai, 2015 umeongezeka hadi asilimia 10.6 kutoka asilimia 10.1 ilivyokuwa mwezi Juni, 2015.

Pata taarifa kamili hapa...