CPI Aprili 2015 (Kiswahili)

Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa kipimo cha mwaka unapima kiwango cha badiliko la kasi ya bei za bidhaa na huduma zote zinazotumiwa na kaya binafsi.

Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa mwezi Aprili, 2015 umeongezeka kidogo hadi asilimia 4.5 kutoka asilimia 4.3 ilivyokuwa mwezi Machi, 2015.

Hii inamaanisha kuwa, kasi ya upandaji wa bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia mwezi Aprili, 2015 imeongezeka ikilinganishwa na kasi iliyokuwepo kwa mwaka ulioishia Machi Februari, 2015.

Fahirisi za Bei zimeongezeka hadi 157.21 kwa mwezi Aprili, 2015 kutoka 150.50 mwezi Aprili, 2014.

Mfumuko wa Bei wa bidhaa za Vyakula na Vinywaji Baridi kwa mwezi Aprili, 2015 umeongezeka hadi asilimia 7.1 kutoka asilimia 5.9 ilivyokuwa mwezi Machi, 2015.

Pata taarifa kamili hapa...