CPI Februari 2015 (Kiswahili)

Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa kipimo cha mwaka unapima kiwango cha badiliko la kasi ya bei za bidhaa na huduma zote zinazotumiwa na kaya binafsi.

Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa mwezi Februari, 2015 umeongezeka kidogo hadi asilimia 4.2 kutoka asilimia 4.0 ilivyokuwa mwezi Januari, 2015.

Hii inamaanisha kuwa, kasi ya upandaji wa bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia mwezi Februari, 2015 imeongezeka kidogo ikilinganishwa na kasi iliyokuwepo kwa mwaka ulioishia mwezi Januari, 2015.

Fahirisi za Bei zimeongezeka hadi 154.83 kwa mwezi Februari, 2015 kutoka 148.62 mwezi Februari, 2014.

Mfumuko wa Bei wa bidhaa za Vyakula na Vinywaji Baridi kwa mwezi Februari 2015 umeongezeka kwa kasi ya asilimia 4.9 kama ilivyokuwa mwezi Januari, 2015.

Pata taarifa kamili hapa...