CPI Januari 2015 (Kiswahili)

Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa kipimo cha mwaka unapima kiwango cha badiliko la kasi ya bei za bidhaa na huduma zote zinazotumiwa na kaya binafsi.

Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa mwezi Januari, 2015 umeendelea kupungua hadi asilimia 4.0 kutoka asilimia 4.8 ilivyokuwa mwezi Desemba, 2014.

Hii inamaanisha kuwa, kasi ya upandaji wa bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia mwezi Januari, 2015 imeendelea kupungua ikilinganishwa na kasi iliyokuwepo kwa mwaka ulioishia mwezi Desemba, 2014. Fahirisi za Bei zimeongezeka hadi 152.43 kwa mwezi Januari, 2015 kutoka 146.60 mwezi Januari, 2014. Mfumuko wa Bei wa bidhaa za Vyakula na Vinywaji Baridi umepungua hadi asilimia 4.9 mwezi Januari 2015 kutoka asilimia 5.7 mwezi Desemba, 2014.

Pata taarifa kamili hapa...