CPI Novemba 2014 (Kiswahili)

Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa kipimo cha mwaka unapima kiwango cha badiliko la kasi ya bei za bidhaa na huduma zote zinazotumiwa na kaya binafsi.

Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa mwezi Novemba, 2014 umepungua zaidi hadi asilimia 5.8 kutoka asilimia 5.9 ilivyokuwa mwezi Oktoba, 2014.

Hii inamaanisha kuwa, kasi ya upandaji wa bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia mwezi Novemba, 2014 imepungua ikilinganishwa na kasi iliyokuwepo kwa mwaka ulioishia mwezi Oktoba, 2014.

Fahirisi za Bei zimeongezeka hadi 150.54kwa mwezi Novemba, 2014 kutoka 142.23 mwezi Novemba, 2013. Mfumuko wa Bei wa bidhaa za Vyakula na Vinywaji Baridi umepungua hadi asilimia 7.0 mwezi Novemba 2014 kutoka asilimia 7.1 mwezi Oktoba, 2014.


Kwa taarifa kamili endelea hapa