CPI Oktoba 2014 (Kiswahili)

Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa kipimo cha mwaka unapima kiwango cha badiliko la kasi ya bei za bidhaa na huduma zote zinazotumiwa na kaya binafsi.

Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa mwezi Oktoba, 2014 umepungua hadi  asilimia 5.9 kutoka asilimia 6.6 ilivyokuwa mwezi Septemba, 2014. Hii inamaanisha kuwa, kasi ya upandaji wa bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia mwezi Oktoba, 2014 imepungua ikilinganishwa na kasi iliyokuwepo kwa mwaka ulioishia mwezi Septemba, 2014.

Fahirisi za Bei zimeongezeka hadi 149.70 kwa mwezi Oktoba, 2014 kutoka 141.39 mwezi Oktoba, 2013. Mfumuko wa Bei wa bidhaa za Vyakula na Vinywaji Baridi umepungua hadi asilimia 7.1 mwezi Oktoba 2014 kutoka asilimia 8.5 ilivyokuwa mwezi Septemba, 2014.

Kwa taarifa kamili endelea hapa