CPI Septemba 2014 (Kiswahili)

Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa kipimo cha mwaka unapima kiwango cha badiliko la kasi ya bei za bidhaa na huduma zote zinazotumiwa na kaya binafsi.

Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa mwezi Septemba, 2014 umepungua hadi asilimia 6.6 kutoka asilimia 6.7 ilivyokuwa mwezi Agosti, 2014.

Hii inamaanisha kuwa, kasi ya upandaji wa bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia mwezi Septemba, 2014 imepungua ikilinganishwa na kasi iliyokuwepo kwa mwaka ulioishia mwezi Agosti, 2014. Fahirisi za Bei  zimeongezeka hadi 149.93 kwa mwezi Septemba, 2014 kutoka 140.61 mwezi Septemba, 2013. Mfumuko wa Bei wa bidhaa za Vyakula na Vinywaji Baridi umepungua hadi asilimia 8.5 mwezi Septemba 2014 kutoka asilimia 8.8 ilivyokuwa mwezi Agosti, 2014.

Kwa taarifa kamili endelea hapa