Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa kipimo cha mwaka unapima kiwango cha badiliko la kasi ya bei za bidhaa na huduma zote zinazotumiwa na kaya binafsi.

Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa mwezi Oktoba, 2015 umeongezeka hadi asilimia 6.3 kutoka asilimia 6.1 ilivyokuwa mwezi Septemba, 2015.

Hii inamaanisha kuwa, kasi ya upandaji wa bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia mwezi Oktoba, 2015 imeongezeka ikilinganishwa na kasi iliyokuwepo kwa mwaka ulioishia mwezi Septemba, 2015. Fahirisi za Bei zimeongezeka hadi 159.17 kwa mwezi Oktoba, 2015 kutoka 149.70 mwezi Oktoba, 2014.

Mfumuko wa Bei wa bidhaa za Vyakula na Vinywaji Baridi kwa mwezi Oktoba, 2015 umeongezeka hadi asilimia 10.2 kutoka asilimia 9.6 ilivyokuwa mwezi Septemba, 2015.

Pata taarifa kamili hapa...