Mfumuko wa Bei - Novemba 2015

Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa kipimo cha mwaka unapima kiwango cha badiliko la kasi ya bei za bidhaa na huduma zote zinazotumiwa na kaya binafsi.

Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa mwezi Novemba, 2015 umeongezeka hadi asilimia 6.6 kutoka asilimia 6.3 ilivyokuwa mwezi Oktoba, 2015.

Hii inamaanisha kuwa, kasi ya upandaji wa bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia mwezi Novemba, 2015 imeongezeka ikilinganishwa na kasi iliyokuwepo kwa mwaka ulioishia mwezi Oktoba, 2015. Fahirisi za Bei zimeongezeka hadi 160.49 kwa mwezi Novemba, 2015 kutoka 150.54 mwezi Novemba, 2014. Mfumuko wa Bei wa bidhaa za Vyakula na Vinywaji Baridi kwa mwezi Novemba, 2015 umeongezeka hadi asilimia 11.2 kutoka asilimia 10.2 ilivyokuwa mwezi Oktoba, 2015.

Pata taarifa kamili hapa...