Mfumuko wa Bei - Desemba 2015

Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa mwezi Desemba, 2015 umeongezeka hadi asilimia 6.8 kutoka asilimia 6.6 ilivyokuwa mwezi Novemba, 2015.

Hii inamaanisha kuwa, kasi ya upandaji wa bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia mwezi Desemba, 2015 imeongezeka ikilinganishwa na kasi iliyokuwepo kwa mwaka ulioishia mwezi Novemba, 2015. Fahirisi za Bei zimeongezeka hadi 161.24 kwa mwezi Desemba, 2015 kutoka 150.92 mwezi Desemba, 2014. Mfumuko wa Bei wa bidhaa za Vyakula na Vinywaji Baridi kwa mwezi Desemba, 2015 umepungua kidogo hadi asilimia 11.1 kutoka asilimia 11.2 ilivyokuwa mwezi Novemba, 2015

Pata taarifa kamili hapa...