Mfumuko wa Bei Mei 2016

Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa kipimo cha mwaka unapima kiwango cha kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma zote zinazotumiwa na kaya binafsi.

Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa mwezi Mei, 2016 umeongezeka kidogo hadi asilimia 5.2 kutoka asilimia 5.1 ilivyokuwa mwezi Aprili, 2016.

Hii inamaanisha kuwa, kasi ya upandaji wa bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia mwezi Mei, 2016 imeongezeka ikilinganishwa na kasi iliyokuwepo kwa mwaka ulioishia mwezi Aprili, 2016.

Fahirisi za Bei zimeongezeka hadi 103.00 mwezi Mei, 2016 kutoka 97.91 mwezi Mei, 2015.  

Pata taarifa kamili hapa...