Mfumuko wa Bei kwa mwezi Agosti 2016

Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa mwezi Agosti, 2016 umepungua hadi asilimia 4.9 kutoka asilimia 5.1 ilivyokuwa mwezi Julai, 2016. Hii inamaanisha kuwa, kasi ya upandaji wa bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia mwezi Agosti, 2016 imepungua ikilinganishwa na kasi iliyokuwepo kwa mwaka ulioishia mwezi Julai, 2016. Fahirisi za Bei zimeongezeka hadi 103.28 mwezi Agosti, 2016 kutoka 98.49 mwezi Agosti, 2015. Mfumuko wa Bei wa bidhaa za Vyakula na Vinywaji Baridi mwezi Agosti, 2016 umepungua hadi asilimia 7.0 kutoka asilimia 7.6 ilivyokuwa mwezi Julai, 2016.  

Pata taarifa kamili hapa