Mfumuko wa Bei kwa mwezi Oktoba 2016

Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa mwezi Oktoba, 2016 umebaki kuwa asilimia 4.5 kama ilivyokuwa mwezi Septemba, 2016.

Hii inamaanisha kuwa, kasi ya upandaji wa bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia mwezi Oktoba, 2016 imekuwa sawa na kasi ya upandaji wa bei ilivyokuwa kwa mwaka ulioishia mwezi Septemba, 2016.

Fahirisi za Bei zimeongezeka hadi 103.17 mwezi Oktoba, 2016 kutoka 98.72 mwezi Oktoba, 2015. Mfumuko wa Bei wa bidhaa za Vyakula na Vinywaji Baridi kwa mwezi Oktoba, 2016 umebaki kuwa asilimia 6.0 kama ilivyokuwa mwezi Septemba, 2016.

Pata Taarifa kamili hapa