Mfumuko wa Bei wa mwezi Desemba 2016

Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa mwezi Desemba, 2016 umeongezeka hadi kufikia asilimia 5.0 kutoka asilimia 4.8 mwezi Novemba, 2016. Hii inamaanisha kuwa, kasi ya upandaji wa bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia mwezi Desemba, 2016 imeongezeka ikilinganishwa na kasi ya upandaji ilivyokuwa kwa mwaka ulioishia mwezi Novemba, 2016. Fahirisi za Bei zimeongezeka hadi 105.04 mwezi Desemba, 2016 kutoka 100.00 mwezi Desemba, 2015. Mfumuko wa Bei wa bidhaa za Vyakula na Vinywaji Baridi kwa mwezi Desemba, 2016 umeongezeka hadi asilimia 7.0 kutoka asilimia 6.2 ilivyokuwa mwezi Novemba, 2016.  

Kwa taarifa kamili bonyeza hapa