Mfumuko wa Bei wa mwezi Januari, 2017

Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa mwezi Januari, 2017 umeongezeka hadi kufikia asilimia 5.2 kutoka asilimia 5.0 mwezi Desemba, 2016. Hii inamaanisha kuwa, kasi ya upandaji wa bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia mwezi Januari, 2017 imeongezeka ikilinganishwa na kasi ya upandaji ilivyokuwa kwa mwaka ulioishia mwezi Desemba, 2016. Fahirisi za Bei zimeongezeka hadi 105.92 mwezi Januari, 2017 kutoka 100.71 mwezi Januari, 2016. Mfumuko wa Bei wa bidhaa za Vyakula na Vinywaji Baridi kwa mwezi Januari, 2017 umeongezeka hadi asilimia 7.6 kutoka asilimia 7.0 ilivyokuwa mwezi Desemba, 2016.  

Kwa taarifa kamili bonyeza hapa