Mfumuko wa Bei wa mwezi Februari, 2017

Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa mwezi Februari, 2017 umeongezeka hadi kufikia asilimia 5.5 kutoka asilimia 5.2 mwezi Januari, 2017. Hii inamaanisha kuwa, kasi ya upandaji wa bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia mwezi Februari, 2017 imeongezeka ikilinganishwa na kasi ya upandaji ilivyokuwa kwa mwaka ulioishia mwezi Januari, 2017. Fahirisi za Bei zimeongezeka hadi 106.97 mwezi Februari, 2017 kutoka 101.44 mwezi Februari, 2016. 

Kwa taarifa kamili bonyeza hapa