Mfumuko wa Bei kwa mwezi Aprili, 2017

Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa mwezi Aprili, 2017 umebaki kuwa asilimia 6.4 kama ilivyokuwa mwezi Machi, 2017. Hii inamaanisha kuwa, kasi ya upandaji wa bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia mwezi Aprili, 2017 imekuwa sawa na kasi ya upandaji ilivyokuwa kwa mwaka ulioishia mwezi Machi, 2017. Fahirisi za Bei zimeongezeka hadi 109.04 mwezi Aprili, 2017 kutoka 102.46 mwezi Aprili, 2016. Mfumuko wa Bei wa bidhaa za Vyakula na Vinywaji Baridi kwa mwezi Aprili, 2017 umeongezeka hadi asilimia 11.8 kutoka asilimia 11.0 ilivyokuwa mwezi Machi, 2017.  

Kwa taarifa kamili bonyeza hapa