Mfumuko wa Bei kwa mwezi Oktoba, 2017

Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa kipimo cha mwaka unapima kiwango cha kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma zote zinazotumiwa na kaya binafsi.

Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa mwezi Oktoba, 2017 umepungua hadi asilimia 5.1 kutoka asilimia 5.3 mwezi Septemba, 2017.

Hii inamaanisha kuwa, kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia mwezi Oktoba, 2017 imepungua ikilinganishwa na kasi ilivyokuwa kwa mwaka ulioishia mwezi Septemba, 2017. Fahirisi za Bei zimeongezeka hadi 108.41 mwezi Oktoba, 2017 kutoka 103.17 mwezi Oktoba, 2016. Mfumuko wa Bei wa bidhaa za Vyakula na Vinywaji Baridi kwa mwezi Oktoba, 2017 umepungua hadi asilimia 8.8 kutoka asilimia 9.3 ilivyokuwa mwezi Septemba, 2017.

Kwa taarifa kamili bonyeza hapa