Mfumuko wa Bei kwa mwezi Novemba 2017

Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa kipimo cha mwaka unapima kiwango cha kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma zote zinazotumiwa na kaya binafsi.

Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa mwezi Novemba, 2017 umepungua hadi asilimia 4.4 kutoka asilimia 5.1 mwezi Oktoba, 2017. Hii inamaanisha kuwa, kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia mwezi Novemba, 2017 imepungua ikilinganishwa na kasi ilivyokuwa kwa mwaka ulioishia mwezi Oktoba, 2017.

Fahirisi za Bei zimeongezeka hadi 108.94 mwezi Novemba, 2017 kutoka 104.32 mwezi Novemba, 2016. Mfumuko wa Bei wa bidhaa za Vyakula na Vinywaji Baridi kwa mwezi Novemba, 2017 umepungua hadi asilimia 7.4 kutoka asilimia 8.8 ilivyokuwa mwezi Oktoba, 2017.  

Kwa taarifa kamili bonyeza hapa