Mfumuko wa Bei kwa mwezi Desemba 2017

Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa kipimo cha mwaka unapima kiwango cha kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma zote zinazotumiwa na kaya binafsi.  Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa mwezi Desemba, 2017 umepungua hadi asilimia 4.0 kutoka asilimia 4.4 mwezi Novemba, 2017. Hii inamaanisha kuwa, kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia mwezi Desemba, 2017 imepungua ikilinganishwa na kasi ilivyokuwa kwa mwaka ulioishia mwezi Novemba, 2017. Fahirisi za Bei zimeongezeka hadi 109.21 mwezi Desemba, 2017 kutoka 105.04 mwezi Desemba, 2016. Mfumuko wa Bei wa bidhaa za Vyakula na Vinywaji Baridi kwa mwezi Desemba, 2017 umepungua hadi asilimia 6.2 kutoka asilimia 7.4 ilivyokuwa mwezi Novemba, 2017.  

Kwa taarifa kamili bonyeza hapa