Mhe. Makinda Akutana, Kufanya Mazungumzo, Profesa Chijoriga
Mwenyekiti wa Bodi ya Usimamizi ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu Mhe. Anne Semamba Makinda akiwa ameambatana na Mtakwimu Mkuu wa Serikali, Dkt. Amina Msengwa wamekutana na kufanya mazungumzo na Mkuu wa Shule ya Uongozi ya Mwalimu Julius Nyerere - MJNLS, Prof. Marcellina Chijoriga ofisini kwake Kibaha mkoani Pwani tarehe 19 Aprili 2026.