Majaribio Utafiti wa NPS 2026 Kimandolu
Timu ya watakwimu kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu - NBS kwa kushirikiana na Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali Zanzibar - OCGS tarehe 12 Mei 2026 imefika katika Mtaa wa Tindigani, Kata ya Kimandolu Halimashauri ya Jiji la Arusha ikiendelea na zoezi la majaribio ya nyenzo zitakazotumika katika Utafiti rasmi wa Kufuatilia Kaya (National Panel Survey (NPS)) Awamu ya Sita 2026 wenye lengo la kubaini maendeleo ya kaya nchini.
Ambapo kwa awamu hiyo Utafiti wa majaribio unafanyika katika Mkoa wa Arusha, Wilaya za Monduli, Arumeru na Arusha Mjini ili kuweza kujaribu nyenzo za utafiti wa NPS ikiwemo vifaa, dodoso na mpangilio wake kwa lengo la kuona kama zinaeleweka kwa Wananchi.
Utafiti rasmi unatarajiwa kuanza mwezi Juni 2026 utafanyika Tanzania Bara na Zanzibar.