Mhe. Makinda Akutana, Kufanya Mazungumzo, Profesa Chijoriga
Mhe. Makinda Akutana, Kufanya Mazungumzo, Profesa Chijoriga
Posted On: 21 April, 2026
Mwenyekiti wa Bodi ya Usimamizi ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu Mhe. Anne Semamba Makinda akiwa ameambatana na Mtakwimu Mkuu wa Serikali, Dkt. Amina Msengwa wamekutana na kufanya mazungumzo na Mkuu wa Shule ya Uongozi ya Mwalimu Julius Nyerere - MJNLS, Prof. Marcellina Chijoriga ofisini kwake Kibaha mkoani Pwani tarehe 19 Aprili 2026.
Pamoja na mambo mengine, viongozi hao wamezungumza kuhusu uongozi bora na namna viongozi wanavyoweza kutumia Takwimu rasmi kufanya maamuzi sahihi ili kuchochea Maendeleo nchini.