NBS Accessibility Tools
NBS Accessibility Tools

Text Size

Language

AASS 2023/2024 Women's Empowerment and Nutrition Module: WEN Tanzania Gender and Environment Survey: TGES 2025 Utafiti wa Kufuatilia Kaya (National Panel Survey, Wave 6: NPS 2026 Tanzania Inflation Rate April 2026: 4.0 %
The United Republic of Tanzania

National Bureau of Statistics

NBS Yaanza Majaribio Utafiti wa Kufuatilia Kaya
Posted On: 11 May, 2026
NBS Yaanza Majaribio Utafiti wa Kufuatilia Kaya

Ofisi ya Taifa ya Takwimu - NBS kwa kushirikiana na Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali Zanzibar - OCGS inatekeleza zoezi la majaribio ya nyenzo zitakazotumika katika Utafiti rasmi wa Kufuatilia Kaya (National Panel Survey (NPS)) Awamu ya Sita 2026.

Akizungumza uwandani katika Kijiji cha Mlimani, Kata ya Engutoto wilayani Monduli tarehe 10 Mei 2026, Mratibu wa Utafiti huo kutoka NBS, Jocelyne Rwehumbiza amesema kwa awamu hiyo Utafiti wa majaribio unafanyika katika Mkoa wa Arusha, Wilaya za Monduli, Alumeru na Arusha Mjini ili kuweza kujaribia nyenzo za utafiti wa NPS ikiwemo vifaa, dodoso na mpangilio wake kwa lengo ya kuona kama zinaeleweka kwa Wananchi.

Naye, Mratibu Msaidizi kutoka OCGS, Khamis Abdul-Rahman Mshamu ameeleza kuwa Utafiti huo umeanza mwaka 1995 na kwa mwaka 2026 ni awamu ya sita ukihusisha kaya ambazo zimechagulia kutoka Mwaka 1995 kuzifuatilia na kuweza kujua maendeleo yake kutoka awamu moja hadi nyingine.

“Utafiti rasmi utakapofanyika unatarajia kutoa viashiria mbalimbali kuhusu maswala ya afya, elimu na hali halisi ya Wananchi ilivyokua kutoka mwaka 1995 hadi 2026.” Amesema Mshamu.

Utafiti huo ambao unatarajiwa kuanza Mwezi juni 2026 utafanyika Tanzania Bara na Zanzibar.