NBS Accessibility Tools
NBS Accessibility Tools

Text Size

Language

AASS 2023/2024 Women's Empowerment and Nutrition Module: WEN Tanzania Gender and Environment Survey: TGES 2025 Utafiti wa Kufuatilia Kaya (National Panel Survey, Wave 6: NPS 2026 Tanzania Inflation Rate April 2026: 4.0 %
The United Republic of Tanzania

National Bureau of Statistics

NBS Yajipanga Kuanzisha Kliniki Tembezi ya Takwimu, SG Apongeza e-Utendaji
Posted On: 11 May, 2026
NBS Yajipanga Kuanzisha Kliniki Tembezi ya Takwimu, SG Apongeza e-Utendaji

Ofisi ya Taifa ya Takwimu - NBS imejipanga kuanzisha Kiliniki Tembezi ya Takwimu ili kuhakikisha Takwimu zinazozalishwa na Ofisi hiyo zinawafikia wahusika na zinatumika ipasavyo katika mipango mbalimbali ya maendeleo badala ya takwimu hizo kubaki makabatini.

Kauli hiyo imetolewa na Mtakwimu Mkuu wa Serikali - SG, Dkt. Amina Msengwa alipokuwa akifungua mafunzo ya siku moja ya kuwajengea uwezo Watumishi wa Ofisi hiyo kuhusu utendaji kazi katika utumishi wa umma ambayo yanaratibiwa na Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, yaliyofanyika kwenye Ukumbi wa Ngorngoro uliopo katika Jengo la Makao Makuu ya NBS jijini Dodoma tarehe 10 Mei 2026.

“Binafsi naipongeza sana Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kwa kuanzisha Mobile Clinic (Kliniki Tembezi) ya kutujengea uwezo ili kuboresha utendaji kazi wetu...programu hii imeanzishwa ni wakati muafaka na sisi tunaiona kuwa ipo haja kuanzisha Mobile Clinic ya Takwimu ili kuhakikisha miongozo tunayoiandaa inawafikia walaji, wadau, wazalishaji wa Takwimu, kuhakikisha Takwimu wanazozalisha zina ubora wa hali ya juu. Amesema Dkt. Msengwa na kuongeza;

“Kwa hiyo sasa na sisi tutakuwa na hizo Mobile Clinic, kuhakikisha kwamba sekta wanazozalisha Takwimu wanaweza kupata hiyo miongozo lakini pia wanaweza kupata matokeo ambayo sasa tunasema hayatakaa makabatini tena, matekeo haya ni kwa ajili ya kuhakikisha kila mtu anajipima, anajitathmini lakini pia anaweka mipango ambayo ina ushahidi wa kitakwimu.”

Pia, Dkt. Msengwa ameupongeza Mfumo wa e-Utendaji na ameiomba Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, ili Mfumo huo uweze kuoana na Mfumo Jumuishi wa Takwimu wa Taifa kwa lengo la kurahisisha upatikanaji rahisi wa taarifa za kiutumishi.

Akizungumza awali kwa niaba ya Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Oswin Mkinga amesema lengo kubwa la mafunzo hayo ni kuwafikia watumishi wote ili kuhuisha usimamizi wa utendaji kazi katika utumishi wa umma hususan kuoanisha majukumu ya kila siku ya mtumishi wa umma na mipango ya Taifa.

“Hii ndiyo Ofisi yetu ya Taifa ya Takwimu...ndiyo Ofisi yenye dhamana ya Takwimu zote hapa nchini na ndiyo standard (viwango) ya Takwimu zetu tunazitoa hapa, kwa hiyo tunapozungumza tunataka tuone namna gani tunaweza kuboresha zaidi utendaji wetu pamoja na namna tunafanya vizuri lakini tunaweza kuboresha zaidi.” Amesema Mkinga.

Aidha, Mkinga amefafanua na kusisitiza umuhimu wa watumishi wa umma kuwekeza miradi yao binafsi ili wakistaafu waishi maisha ya furaha kwa kuwa na kipato chao nje ya pensheni.

Jambo jingine alilosisitiza Mkinga ni kuhusu umuhimu wa matumizi sahihi ya Mfumo wa e-Utendaji kwa maana ya Mfumo wa Taarifa za Usimamizi wa Utendaji wa Wafanyakazi wa Umma – PEPMIS.

Nbs Yajipanga Kuanzisha Kliniki Tembezi ya Takwimu, SG Apongeza e-Utendaji  