The United Republic of Tanzania

National Bureau of Statistics

Statistics for Development
SG Dkt. Msengwa Apokea Mpango Kazi Tathmini ya NSS
Posted On: 28 January, 2026
SG Dkt. Msengwa Apokea Mpango Kazi Tathmini ya NSS

Mtakwimu Mkuu wa Serikali, Dkt. Amina Msengwa amepokea mpango kazi wa zoezi la Tathmini ya Mfumo wa Takwimu nchini ambao umewasilishwa na Timu ya Tathmini ya Mpango huo ofisini kwake jijini Dodoma leo tarehe 28 Januari 2026.

Aidha, mchakato wa tathmini ya Mfumo wa Taifa wa Takwimu (National Statistical System – NSS), umezinduliwa rasmi na Naibu Katibu Mkuu Usimamizi wa Fedha za Umma, Wizara ya Fedha, Amina Khamis Shaaban kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Natu El-maamry Mwamba tarehe 27 Januari 2026.