Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Taifa ya Takwimu

Takwimu kwa Maendeleo
Sensa 2022

Sensa ya Mwaka 2022 ni ya sita tangu kuasisiwa kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwaka 1964. Sensa zilizotangulia zilifanyika mwaka 1967, 1978, 1988, 2002 na 2012. Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022 ni Sensa ya kwanza kufanyika kidijitali nchini Tanzania na imefanyika kwa mafanikio makubwa na kuwezesha kutoa matokeo kwa wakati.